Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa beki kisiki na nahodha wa Yanga Lamine Moro
Ni mchezaji kiongozi wa mfano, anayejitoa muda wote kuipigania timu
Mpaka sasa amekuwa na msimu mzuri akiwa miongoni mwa vinara wa mabao katika kikosi cha Yanga, amefunga mabao manne
Ni Deusi Kaseke pekee aliyefunga mabao mengi kuliko yale aliyoweka kibindoni Lamine (Kaseke kafunga matano)
Lamine anaongoza safu bora ya ulinzi ambayo haijapoteza mchezo katika mechi 35 walizocheza mfululizo kwenye ligi kuanzia msimu uliopita
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii muhimu ya kumbukumbu kwake
HAPPY BIRTHDAY LAMINE...!
ADVERTISE HERE