Tambeni, tembeeni kifua mbele bado tuko juu - Nugaz

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Feb 2021
Tambeni, tembeeni kifua mbele bado tuko juu - Nugaz

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz ameeleza kushangazwa na 'unyonge' unaoonyeshwa na mashabiki baada ya timu kulazimishwa sare ya bao 1-1 mkoani Mbeya dhidi ya Mbeya City juzi

Aidha, Nugaz amewataka mashabiki kutokubali kuaminishwa kuwa wana timu dhaifu kwani mpaka sasa Yanga ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo msimu huu

"Mwanachama,mpenzi na shabiki wa Yanga kwanini ukajikosesha amani kwa timu kutoka sare na kuaminishwa kuwa timu haitopata matokeo na wewe unaamini hilo?," alihoji Nugaz

"Kumbuka mpaka sasa tuko kileleni (Namba moja) kwenye msimamo wa ligi na pia tukiwa na rekodi sahihi ya kutopoteza Mchezo hata mmoja"

"Lazima tukubaliane na matokeo ya Mpira na sio kulaumu sana kana kwamba tuko nafasi ya 8 au tunaburuza mkia"

"Tambeni Mtaani msitembee kinyonge,vimbeni mtaani na muendelee kuipa hamasa timu yetu Insha Allah kila kitu kitaenda Sawa"

"Kisha tukutane Uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumatano kwenye Mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar saa 1 Kamili usiku Tujitokeze kwa wingi bila kukosa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’