Uongozi wa klabu ya Yanga umesema watachukua hatua juu ya 'dhihaka' iliyofanywa na Afisa Habari wa Simba Haji Manara kwa 'brand' ya klabu ya Yanga na wadhamini wake
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema wamempa siku 14 Manara ajieleze ikiwa ni pamoja na kuwaomba radhi Wanayanga kwa tukio la kuidhalilisha nembo ya klabu na kama sivyo watamfikisha Mahakamani
"Tulimuwasilishia wito Haji Manara ambao anapaswa kuujibu ndani ya siku 14. Anapaswa kuja kutuomba radhi na kama hatafanya hivyo basi tutamfikisha Mahakamani kwa tukio la kuchezea nembo ya klabu ya Yanga," amesema Mwakalebela
"Mtu huyu amekuwa na tabia ya kudhihaki sana brand yetu mpaka ametuletea matatizo na mdhamini wetu. Tumemfikisha kwa TFF pia hatua zichukuliwe na iwe fundisho kwa wengine"
Hivi karibuni Manara aliondoa chapisho alilokuwa amebandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ambalo lililenga kuidhalilisha 'brand' ya Yanga pamoja na wadhamini wake
Kwa wingi wao, mashabiki wa Yanga walionesha kukerwa na chapisho hilo, waliutaka uongozi wa Yanga kumchukulia hatua Manara ambaye kwake imekuwa kawaida kuichezea brand ya Yanga pasipo kujali athari ya matukio anayofanya ambayo mwenyewe amedai ni ya utani wa jadi