Shikhalo kupewa muda zaidi wa kucheza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Feb 2021
Shikhalo kupewa muda zaidi wa kucheza

Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze ameeleza kuvutiwa na kiwango kilichoonyeshwa na mlinda lango Farouk Shikhalo katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar, mchezo ambao Yanga ilifanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0

Huo ulikuwa mchezo wa pili Shikhalo anacheza kwenye ligi msimu huu akichukua nafasi ya Metacha Mnata ambaye jana alipumzishwa

Kaze amesema katika duru ya pili Shikhalo atapewa nafasi zaidi ya kucheza kama ilivyokuwa kwa Metacha ambaye amecheza jumla ya michezo 19

"Metacha hana tatizo lolote, tuliamua kumpumzisha kwani ametumika kwa mechi nyingi. Shikhalo amefanya vizuri pia nafikiri tutampa mechi zaidi katika duru hii pamoja na kumtumia kwenye michuano ya kombe la FA," alisema Kaze

Mlinda lango huyo kutoka nchini Kenya alirejesha imani ya mabosi wake kwake kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi iliyofanyika mwezi uliopita visiwani Zanzibar

Katika michuano hiyo, Shikhalo aliibuka kuwa mlinda lango bora wa mashindano, akiisaidia Yanga kushinda mechi za nusu fainali dhidi ya Azam Fc na fainali dhidi ya Simba kupitia mikwaju ya penati

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’