Beki kisiki wa Yanga Kelvin Yondani atakuwa nje akiendelea kuuguza jajeraha yake mpaka Disemba 28.
Yondani aliumia wakati akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' kwenye michuano ya Chalenji nchini Kenya.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema daktari wa timu Dk Edward Bavu ameuhakikishia uongozi kuwa Yondani atakuwa tayari kurejea dimbani Disemba 28 ikiwa ni siku moja kabla ya kuivaa Mbao FC mkoani Mwanza.
Aidha Ten amesema mshambuliaji Amissi Tambwe yuko fiti kwa asilimia 100 huku Thabani Kamusoko akianza mazoezi maalumu ya kuweza kumrejesha dimbani haraka.
Donald Ngoma naye anatarajiwa kurejea dimbani mwishoni mwa mwezi huu.

ADVERTISE HERE