Wanayanga kushirikishwa ukarabati wa Jengo Makao Makuu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Mar 2021
Wanayanga kushirikishwa ukarabati wa Jengo Makao Makuu

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amewataka wapenzi, Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kuunga mkono juhudi za ukarabati wa Jengo la Makao Makuu lililoko Mtaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam

Tawi la Yanga 'Elite' liliendesha zoezi la kupaka rangi jengo hilo lenye historia kubwa, Dk Msolla amewataka Wanayanga wengine waunge mkono juhudi hizo kwa kujitolea kufanya ukarabati katika maeneo mengine

Akizungumza na Wanahabari mapema leo, Dk Msolla amesema wanakusudia kulitumia jengo hilo kwa ajili ya kambi za timu ya Vijana na ile ya Wanawake 'Yanga Princess' hivyo wanahitaji kukarabati miundo mbinu ya jengo hilo ili liweze kutumika ipasavyo

"Ukarabati wa jengo la Yanga utafanywa na wanayanga wenyewe, tunafurahia kuna tawi moja (Elite) limejitokeza kupiga rangi jengo letu la Makao Makuu"

"Matawi mengine yaige kutoka kwa tawi la Elite kwani kinachofuata sasa ni kukarabati vyumba vya ndani na tunaamini wananchi ni wengi na kazi hiyo watafanya wenyewe"

"Yanga tuna timu nne, gharama za kuweka timu kambini kwa maana ya kulipia hoteli ni kubwa sana. Tukishakarabati jengo letu timu zetu za U17, U20 na Yanga Princess zitakuwa zinakaa kwenye jengo letu zinapokuwa na mashindano," amesema Dk Msolla

Gharama za kukarabati chumba kimoja katika jengo hilo zinafikia Tsh Milioni sita

Baadhi ya Wanachama tayari wamejitokeza kufanya ukarabati. Wanachama hao ni pmoja na Thobias Lingalangala, Injinia Hersi Said, martin Komba, Wanachama wa mkoani Geita, Arafat na Afisa Mhamasishaji Antonio Nugaz aliyeahidi kukarabati vyumba viwili

Vyumba vinavyohitaji ukarabati viko 30 lakini pia kuna Gym na kuweka vivutio ili jengo liwe na Hadhi

Kuhusu mradi wa Kigamboni, uongozi wa Yanga unatarajiwa kumtangaza mkandarasi wa mradi huo wiki ijayo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’