Kesho Jumapili, kikosi cha Yanga kitashuka kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuikabili Polisi Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union, mechi ya Polisi Tanzania ni ya lazima kwa Yanga kuondoka na alama zote tatu ili kuweka hai matumaini ya kutwaa ubingwa msimu huu
Yanga iliwasili Arusha jana jioni wakipata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wao licha ya kupoteza mchezo uliopita
Yanga itashuka dimba la Sheikh Amri Abeid wakiwa na kikosi chao kamili kilichokuwepo Tanga isipokuwa Michael Sarpong ambaye ni majeruhi
Sarpong alipata majeraha katika mchezo dhidi ya Coastal Union, akitolewa katika mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na Yacouba Songne
Mechi dhidi ya Polisi Tanzania ni ya kufa au kupona...