Inasikitisha sana kuona Yanga imepoteana kwenye duru ya pili licha ya jitihada kubwa zinazofanywa na wadhamini/wahisani GSM
Wachezaji na benchi la ufundi hawana cha kuwaambia mashabiki kwa nini mambo yamekuwa hivi
Kwani wanaishi katika kambi nzuri, wanalipwa mishahara mizuri na wamepatiwa kila walichohitaji
Ni aibu kwa Yanga kushinda mchezo mmoja katika mechi sita zilizopita kwenye ligi
Hiki ni kiwango cha chini sana kwa kikosi cha Yanga ambacho kimeundwa kwa gharama kubwa
Nadhani lipo jambo, wakati huu ligi inaposimama kupisha Afcon Qualification, inapaswa viongozi wakae chini kubaini ilipo shida na waipatie ufumbuzi
Kwa timu inayowania ubingwa, haya sio matokeo yanayoweza kukupa ubingwa
ADVERTISE HERE