Tutaharakisha kupata benchi la ufundi - Mfikirwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Mar 2021
Tutaharakisha kupata benchi la ufundi - Mfikirwa

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa amesema Kamati ya Utendaji inatarajiwa kukutana leo kuandaa mchakato ambao utatumika kupata benchi la ufundi

Mfikirwa amesema timu ilirejea jijini Dar es salaam jana wakitokea mkoani Arusha ambao juzi walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania

Ni matokeo hayo yaliyopelekea kuvunjwa kwa benchi zima la ufundi lililokuwa likiongozwa na kocha Cedric Kaze

Amesema wanatarajia kukamilisha mchakato huo mapema, makocha wanaotajwa kwenye mitandao ya kijamii ni tetesi tu kwa sababu hawajatangaza jina la kocha yeyote ambaye atakuja kurithi mikoba ya Kaze

Amesema baada ya juzi kutoa taarifa ya kuvunja benchi la ufundi, uongozi unatarajia kukutana leo, kwa ajili ya kuweka mambo sawa ikiwamo mchakato ambao utatumika kwa ajili ya kupata benchi zima la ufundi.

"Bado hatujaweka wazi, mchakato upi tutatumia kupata benchi la ufundi, kwa sababu tulitoa taarifa ya kuvunja benchi la ufundi tukiwa Arusha, sasa tunarejea nyumbani na kesho (leo), Kamati ya Utendaji itakutana kwa ajili ya kuangalia mchakato upi ambao tutautumia kupata benchi la ufundi," alisema Mfikirwa

Mfikirwa amesema wanahitaji kufanya mchakato huo mapema ili benchi la ufundi litangazwe hivi karibuni kabla ya ligi kuendelea kushika kasi mzunguko wa pili, ambao kwa sasa itasimama kwa muda wa wiki tatu kupisha kalenda ya michuano ya kimataifa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’