Uzoefu kigezo cha kwanza kocha mpya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Mar 2021
Uzoefu kigezo cha kwanza kocha mpya

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk Mshindo Msolla jana alitangaza kurejeshwa kwa Juma Mwambusi kuwa Kaimu Kocha Mkuu akichukua nafasi ya iliyoachwa na Kocha Cedric Kaze aliyetimuliwa baada ya mchezo dhidi ya Polisi Tanzania uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 mwishoni mwa wiki iliyopita

Dk Msolla alisema kuwa mchakato wa kumtafuta kocha tayari umeanza jukumu hilo likiachwa mikononi mwa Kamati ya Ufundi iliyosheheni Wana taaluma wa soka

Aidha Dk Msolla alidokeza kuwa kwa sasa Wanahitaji kocha mwenye 'CV nzuri' kigezo cha kwanza awe kocha mwenye uzoefu na soka la Afrika ambaye atamudu kufanya kazi katika mazingira ya Tanzania

"Kamati ya ufundi itapokea CV za makocha mbalimbali na wao watachambua kulingana na vigezo ambayo tutakuwa tumeweka. Lakini muhimu kocha tunayemuhitaji sisi awe na uzoefu wa soka la Afrika na ambaye ataweza kufanya kazi katika mazingira yetu," alisema Dk Msolla

Dk Msolla aliongeza kuwa kwa sasa timu itakuwa chini ya Kocha Juma Mwambusi, wana imani kubwa na kocha huyo kwani sio mgeni kwa kikosi hiki cha Yanga msimu huu

"Tumekuwa na Mwambusi tangu mwanzo mwa msimu, aliondoka baada ya michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuugua. Yanga imemsaidia matibabu yake na sasa amepona. Hakuna jambo geni kwake, wachezaji wote anawafahamu, naamini timu itakuwa salama chini yake wakati tunaendelea kutafuta kocha mpya"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’