Klabu ya Yanga imeendelea kupokea CV za makocha ambao wanataka kuchukua nafasi iliyoachwa na kocha Cedric Kaze aliyeondolewa na uongozi hivi karibuni
Hadi kufikia jana, Yanga imepokea CV za makocha 72 ambao wamejitosa kutaka kumrithi Kaze
Afisa Habari wa Yanga amesema wameendelea kupokea CV za makocha hao, Kamati ya Ufundi ikiachiwa jukumu la kuzichambua CV hizo ili kupata majina matatu bora
"Mpaka muda huu tumepokea CV za makocha 72 wakiomba kazi ya kuinoa Yanga, bado tunaendelea kupokea maombi zaidi. Kamati ya Ufundi ndio itakayokuwa na jukumu la kufanya upembuzi ili kupata kocha mwenye sifa tunazozitaka," alisema Bumbuli
Wakati zoezi hilo likiendelea, kocha wa muda Juma Mwambusi tayari ameripoti kambini kuendelea na majukumu yake
ADVERTISE HERE