Stars kamili kuivaa Kenya Jumatatu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Mar 2021
Stars kamili kuivaa Kenya Jumatatu

Timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' kesho Jumatano watashuka kwenye uwanja wa Nyayo nchini Kenya kuikabili Harambee Stars katika mchezo wa kirafiki yakiwa ni maandalizi kuelekea mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afcon 2021 dhidi ya Guinea ya Ikweta

Tanzania iliyowasili Kenya jana, leo jioni ilifanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja huo wa Nyayo

Kocha Mkuu wa Tanzania Kim Poulsen amesema vijana wake wako tayari kuikabili Kenya hapo kesho

"Tumejiandaa vizuri kwa mchezo wa kesho wa kirafiki dhidi ya Kenya. Tumefanya mazoezi ya kupiga pasi, kupokea pasi pia na katika hali ya kawaida timu iko vizuri, tuko tayari kwa kucheza kandanda Safi na kila mchezaji yuko tayari kwa mchezo kutoka na mazoezi yaliyofanyika," alisema Poulsen

Naye Kiungo wa Stars Himid Mao amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo huo

Tanzania itacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Harambee Stars huko Kenya. Baada ya mchezo wa kesho, timu hizo zitarudiana siku tatu baadae katika uwanja wa Kasarani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
45m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’