Azam Fc kujipima na Gor Mahia

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 Mar 2023
Azam Fc kujipima na Gor Mahia

Kikosi cha Azam FC kitacheza mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya, kwa ajili ya kujiandaa na Michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyosalia msimu huu, pamoja na mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya Mtibwa Sugar.

Azam FC imethibitisha uwepo wa mchezo huo kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii, baada ya Benchi la Ufundi kupendekeza kuchezwa kwa michezo hiyo angalau miwili katika kipindi hiki cha Kalenda ya FIFA.

Mchezo huo dhidi ya Gor Mahia umepangwa kuchezwa Jumamosi (Machi 26) katika Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi nchini Kenya.

Kabla ya mchezo huo Azam FC itacheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya JKU kutoka visiwani Zanzibar siku ya Jumatano (Machi 22), katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Benchi la Ufundi Azam FC Dani Cadena amesema wamelazimika kukitumia kipindi hiki kwa mchezo huo, ili kuwaweka sawa wachezaji wao waliosalia kikosini, baada ya wenzao kuitwa kuziwakilisha timu zao za taifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Cadena amesema kutakuwa na muda mrefu kwa wao kutocheza, hivyo wameona ni vyema kutotoa ruhusa ya mapumziko kwa lengo la kurejesha morali ya timu yao baada ya kusuasua hivi karibuni.

"Ruhusa ambayo tumeitoa ni kwa wachezaji walioitwa timu za taifa, wengine wote tutaendelea na mazoezi kwa lengo la kujiweka imara zaidi kutokana na michezo migumu iliyokuwa mbele yetu," amesema Dani Cadena

Mchezo wa mwisho kwa Azam FC ulikuwa ni Machi 13 ilipochapwa bao 1-0 na Ihefu FC kwenye Uwanja wa Highland Estate na baada ya hapo itacheza na Mtibwa Sugar katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ kati ya Aprili 3.

Wachezaji Raia wa Tanzania, Sospeter Bajana na Abdul Suleiman ‘Sopu’ ni wachezaji wa Azam FC walioitwa katika kikosi cha 'Taifa Stars' kilichoelekea Misri tayari kwa mchezo wa kufuzu AFCON 2023 dhidi ya Uganda.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa Machi 24 nchini Misri, kabla ya timu hizo hazijarudiana jijini Dar es salaam Machi 28

Mlinda lango Ali Ahamada yeye amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Comoro

ADVERTISE HERE

More Stories

TFF kusimamia uchaguzi wa Simba, ratiba kuboreshwa
TFF kusimamia uchaguzi wa Simba, ratiba kuboreshwa
12m ago
READ MORE β†’
Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
3h ago
READ MORE β†’
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
3h ago
READ MORE β†’
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
4h ago
READ MORE β†’
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
6h ago
READ MORE β†’
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
19h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
21h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
21h ago
READ MORE β†’