Yanga

Yanga yajipanga kumbakisha Nabi

Joel JJ By Joel JJ
21 Mar 2023
Yanga yajipanga kumbakisha Nabi

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema matunda yanayoonekana sasa ni matokeo ya uwekezaji mkubwa uliofanyika ndani ya klabu hiyo

Arafat amesema wamefanya usajili wa wachezaji bora na benchi la ufundi lililosheheni watu mahiri wakiongozwa na Profesa Nasreddine Nabi ambaye tetesi zimeanza juu ya kuhitajika kwake na vigogo wa soka barani Afrika hasa baada ya kuiongoza Yanga kutinga robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika

Arafat amesema klabu ina malengo ya muda mrefu hivyo haitakubali kocha wake aondoke kirahisi

"Kitu pekee ambacho kinatutofautisha na wapinzani wetu wengi ni kuwa na benchi la ufundi pana lenye wataalam bora"

"Nabi kuondoka linawezekana lakini haiwezi kuwa sasa, nadhani hata yeye anaamini yuko katika klabu ambayo hatua chache zijazo anaweza kuwa katika rekodi kubwa zaidi ya mafanikio," alisema Arafat

"Bado tunamhitaji sana Nabi niwahakikishie mashabiki wetu kwamba kocha wao huyu na mwingine haitakuwa rahisi kwetu kuwaachia, tuna malengo makubwa na hii ni safari tu ya kufika huko"

"Tunafahamu hizi taarifa za sisi kuwa na kocha bora kama Nabi wengine ni ndoto zao, Yanga tuko katika mafanikio haya kutokana na kutumia nguvu kuwaweka wataalam wote bora kama hawa, utulivu wa namna hii klabu zingine hazina ndio maana wanayumba kila wakati"

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
4h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
5h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
7h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
7h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
8h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
8h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
8h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
8h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
9h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
11h ago
READ MORE →