Tanzania - Taifa Stars - Yanga - Simba - Azam

Waamuzi waliomaliza adhabu wabaki katika uangalizi

Joel JJ By Joel JJ
29 Mar 2023
Waamuzi waliomaliza adhabu wabaki katika uangalizi

Licha ya baadhi ya waamuzi kumaliza adhabu zao za kufungiwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Nassor Hamduni amesema wataendelea kuwa chini ya uangalizi maalumu hadi pale watakapojiridhisha

Hamduni alikiri kuwepo kwa waamuzi ambao wamemaliza adhabu walizopewa lakini amesisitiza kwa sasa kuwaweka kwenye ratiba ni mapema hadi pale watakapoona inafaa kuwarejesha.

Mmoja ya waamuzi ambao wamemaliza adhabu ni pamoja na Ahmed Arajiga ambaye alifungiwa miezi sita kutokana na makosa mbalimbali ya kujirudia katika kutafsiri sheria za soka uwanjani

"Bado hatujawarejesha hadi sasa ili tuone namna gani tutafanya hivyo, wanaweza wakarejea uwanjani kama ambavyo nia yetu ilivyo lakini wanaweza wakaonekana msimu ujao"

"Kwa sasa siwezi kufanya tathmini ya kiwango cha waamuzi kama kimeongezeka au kimepungua lakini msimu ukimalizika naweza kufanya hivyo kwa kuangalia ripoti mbalimbali," alisema Hamduni.

Hata hivyo, aliongeza kuna baadhi wamesharudishwa ndio maana kunaonekana kuna ubora katika michezo ya ligi mbalimbali zinazoendelea tofauti na hali ilivyokuwa siku za nyuma.

"Arajiga licha ya kumaliza miezi sita lakini yupo katika uangalizi kama ilivyo kwa kina, Sasii (Elly) na wengine, hivyo tunaomba wadau watuvumilie kidogo," Hamduni alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
15m ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
30m ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
1h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
1h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
1h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
2h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
4h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
14h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
14h ago
READ MORE →