Azam - Local

Azam Fc yatimiza masharti CAF, yainunua Baobab Queens

Joel JJ By Joel JJ
β€’
19 Jun 2023
Azam Fc yatimiza masharti CAF, yainunua Baobab Queens

Klabu ya Azam FC imeingia makubaliano ya kuimiliki Baobab Queens ya Dodoma kwa muda wa mwaka mmoja nili kutimiza sharti la CAF ambao wameagiza klabu zote zitakazoshiriki michuano ya CAF msimu ujao lazima ziwe na timu za Wanawake

Azam kama ilivyokuwa kwa Singida Fountain Gate (zamani Singida BS), zilikata tiketi ya michuano ya kimataifa msimu ujao, lakini zilikuwa zikibanwa na masharti yaliyowekwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) likitaka klabu shiriki zote kulazimika kuwa na timu za soka za wanawake

Singida ilimalizana mapema na Fountain Gate kwa kuuza hisa zao na kubadilisha hadi jina ikiwapa fursa ya kuimiliki timu ya wanawake ya Fountain Gate Princess iliyopo Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) kabla ya Azam nayo kufikia makubaliano maalum na Baobab Queens

Hii hapa taarifa iliyotolewa na Azam Fc;

 "Katika kutekeleza agizo la kikanuni la leseni za vilabu kutoka Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF, Azam FC inayo furaha kuutangazia umma kwamba imeingia makubaliano ya ushirikiano na klabu ya soka la wanawake ya Baobab Queens ya Dodoma.

Kwa mujibu wa kanuni mpya za CAF, klabu yoyote itakayopata nafasi ya kushiriki mashindano ya Afrika kuanzia msimu wa 2023/24, itapaswa aidha kuwa na timu ya wanawake au kushirikiana katika uendeshaji na taasisi nyingine yenye timu ya wanawake.

Kwa makubaliano hayo na Baobab, ni rasmi sasa kwamba klabu hiyo ya Dodoma itakuwa klabu dada ya Azam FC kuanzia msimu ujao"

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
3h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
7h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
7h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
8h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
9h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
9h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
10h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
10h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
1d ago
READ MORE β†’