Yanga - Local

Yanga yaalikwa sherehe za Uhuru Malawi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Jul 2023
Yanga yaalikwa sherehe za Uhuru Malawi

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wamealikwa nchini Malawi kwenye maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa nchi hiyo ambazo zitafanyika Julai 06 2023

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema kwa heshima waliyopewa na Malawi, wamelazimika kuwaita wachezaji kambini kwa ajili ya kuhudhuria mwaliko huo wakiongozana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Samia Suluhu Hassan

Kamwe amesema wachezaji 15 wa kikosi cha kwanza wataambatana na wachezaji wengine sita kutoka timu ya vijana

Kamwe amesema mwaliko huo ni matokeo ya mafanikio ambayo Yanga wamepata katika misimu miwili iliyopita

"Tumepokea mwaliko maalumu kutoka kwa Serikali ya Malawi kucheza mchezo maalumu kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Malawi itakayofanyika Julai 6, 2023. Hii ni heshima ya kipekee kwa Tanzania na klabu ya Yanga kualikwa kwenye sherehe kubwa ya nchi ambayo itawakutanisha marais wa nchi mbalimbali akiwemo Rais wa Tanzania Mama Samia Sluhu Hassan"

"Mwaliko huu unatosha kuonyesha ukubwa wa klabu yetu na heshima ambayo tunapewa huko nje. Kwa mara nyingine tutakwenda Malawi kwa ndege maalum ambayo itaturudisha nchini baada ya mchezo," alitamba Kamwe

Wachezaji wa Yanga wanatarajia kuripoti kambini siku ya kesho Jumanne na timu kuondoka nchini mapema siku ya Jumatano

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
1h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
1h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
2h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
5h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
9h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
9h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
10h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
11h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
12h ago
READ MORE β†’