Simba - Local

Kapombe afunguka kucheza Super Ligi

Joel JJ By Joel JJ
5 Sep 2023
Kapombe afunguka kucheza Super Ligi

Beki wa kulia wa Simba Shomari Kapombe amesema ni heshima kubwa kwa wachezaji na klabu ya Simba kwa ujumla kupata nafasi ya kushiriki michuano ya African Football League (Super League) ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika

Simba ni miongoni mwa timu nane zilizopata nafasi hiyo baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya CAF katika miaka mitano iliyopita

Baada ya droo ya mechi za robo fainali kufanyika na Simba kupangwa kucheza na Al Ahly, Kapombe amesema hawana hofu yoyote juu ya kuwakabili Al Ahly kwani wana rekodi nzuri wanapokutana nyumbani na wababe hao wa soka la Afrika

"Kwanza ni heshima kubwa kwetu wachezaji na klabu ya Simba kupata nafasi ya kuwa miongoni mwa timu nane kubwa barani Afrika kushiriki mashindano haya kwa mara ya kwanza"

"Mechi dhidi ya Al Ahly itakuwa nzuri, katika uwanja wa Benjamin Mkapa historia yetu ni nzuri tunapokutana na Al Ahly, tumeweza kuwafunga mara zote"

"Sisi kama Simba tunajiandaa kufanya vizuri ili tusonge mbele katika mashindano hayo," alisema Kapombe

Kapombe ni mmoja wa wachezaji ambao walikuwemo katika vikosi vya Simba vilivyopata ushindi katika mechi zote dhidi ya Al Ahly katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Wachezaji wengine ni Aishi Manula, Clatous Chama, Mohammed Hussein, nahodha John Bocco, Mzamiru Yassin na Luis Miquissone ambaye alifunga bao la ushindi katika mchezo wa mwisho uliozikutanisha timu hizo uwanja wa Benjamin Mkapa

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
5h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
6h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
8h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
8h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
9h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
9h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
9h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
9h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
10h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
12h ago
READ MORE →