Simba na Mpanzu uhakika dirisha dogo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 19th September 2024


Simba na Mpanzu uhakika dirisha dogo

Winga Elie Mpanzu anahesabu siku tu kabla ya kujiunga na Simba pale dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa mwezi Disemba, imefahamika

Baada ya mvutano wa kimkataba kati yake na AS Vita, Mpanzu sasa ni mchezaji huru baada ya kugomea ofa ya kusaini mkataba mpya kuendelea kuitumikia AS Vita

Alikwenda barani Ulaya kufanya majaribio katika klabu kadhaa lakini hakufanikiwa

Chanzo cha kuaminika kutoka DR Congo, kimethibitisha kuwa Mpanzu atajiunga na Simba

"Mpanzu atakuja huko Tanzania kucheza Simba mwezi Januari. Kulikuwa na shida ya mkataba ndio sababu hakusajiliwa katika dirisha lililopita"

"Lakini kwa sasa ni mchezaji huru, ana makubaliano ya kujiunga na Simba katika dirisha dogo," kilieleza chanzo

Katika dirisha lililopita la usajili, Simba ilifanya jitihada kubwa za kumsajili Mpanzu lakini haikuwezekana baada ya mchezaji huyo kupata mwaliko wa kufanya majaribio Ubelgiji siku chache kabla ya dirisha la usajili kufungwa


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.