Ijumaa ni Derby ya Mapacha Singida

Joel JJ By Joel JJ β€’ 24th October 2024


Ijumaa ni Derby ya Mapacha Singida

Wenyewe wanaiita Pacha Derby! Ni siku ya Ijumaa Oktoba 25 nyasi za uwanja wa CCM Liti mkoani Singida zitawaka moto pale timu 'mapacha' Singida Black Stars na Fountain Gate zitakapoumana

Hii itakuwa mechi ya aina yake ambayo itazikutanisha timu mbili bora katika ligi kuu ya NBC msimu huu

Singida BS iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikikusanya alama 19 baada ya mechi 7 wakati Fountain Gate wako nafasi ya nne wakiwa na alama 16 baada ya mechi 8

Upinzani wa timu hizi ulianza msimu uliopita pale baadhi ya waliokuwa mabosi wa Singida Big Stars kujitoa na kuinunua Ihefu Fc huku wakiondoka na karibu nyota wote wa kigeni waliokuwa wakiitumikia timu hiyo

Baadae Ihefu Fc ikabadili jina na kuitwa Singida Black Stars huku ikihamishia makazi yake Singida

Singida Big Stars ikabadilishwa jina na kuwa Singida Fountain Gate na kuhamishia makazi yake jijini Mwanza yalipokuwa makazi ya wamiliki wapya walioinunua timu hiyo na kuibadili jina kuiita Fountain Gate

Imeitwa Pacha Derby kwa sababu wamiliki wa timu hizi walikuwa pamoja kabla ya sintofahamu iliyojitokeza baada ya Singida Big Stas kuuzwa


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.