International,Normal News,Al Hilal, PSG, Barcelona

Neymar majanga Saudia

Joel JJ By Joel JJ
6 Nov 2024
Neymar majanga Saudia

Wiki mbili baada ya kurejea kutoka kwenye majeraha yaliyomuweka nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi 12, nyota wa Brazil Neymar ameumia paja akiitumikia Al-Hilal kwenye Ligi ya Mabingwa Asia.

Katika dakika ya 58 ya ushindi wa 3-0 wa Al Hilal dhidi ya Esteghlal ya Iran, Neymar aliingia uwanjani lakini hakudumu uwanjani kwa muda mrefu, akatoka tena dakika ya 87 baada ya kwenda chini na kushika nyuma ya mguu wake wa kulia

Mechi dhidi ya Esteghlal ilikuwa mechi ya pili kwa Neymar tangu aliporejea baada ya kupona jeraha la meniscus katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia na Brazil dhidi ya Uruguay

Alirejea uwanjani dhidi ya Al Ain mnamo Oktoba 21. Neymar hawezi kucheza katika Ligi Kuu ya Saudia kwa sasa kwa sababu hajasajiliwa

Katika miaka ya hivi karibuni, Neymar ameandamwa na majeraha ya mara kwa mara. Akiwa Paris Saint-Germain alikumbana na majeraha ya aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na jeraha kubwa la metatarsal, lililomweka nje mara nyingi kati ya 2017 na 2023

Msimu uliopita wa kiangazi, alihama kutoka mji mkuu wa Ufaransa hadi Saudi Arabia kwa mkataba wa miaka miwili na Al-Hilal]

Ada ya uhamisho ilikuwa euro milioni 90. Mnamo 2017, Neymar alijiunga na PSG kutoka FC Barcelona kwa ada ya rekodi ya dunia ya pauni 222 milioni. Kufikia sasa, Mbrazil huyo ameichezea Al Hilal katika mechi saba pekee.

More Stories

Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
25m ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
28m ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
45m ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
48m ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
2h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
13h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
13h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
13h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
17h ago
READ MORE →