Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeshangazwa na taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu uhalali wa mchezaji Muhamed Ame kuchezea timu ya Taifa (Taifa Stars)
Tunapenda kuufahamisha umma kuwa Ame ni miongoni wa wachezaji 23 waliokuwa wameorodheshwa kwa ajili ya mechi dhidi ya Guinea. Kabla ya mechi hiyo, wachezaji wa Stars walikaguliwa na timu pinzani pamoja na Kamishna ambapo waliruhusiwa kucheza
Mechi hiyo ya mchujo ya AFCON ilichezwa Dar es Salaam ambapo Stars ilishinda bao 1-0, hivyo kufuzu kucheza fainali
TFF haina taarifa yoyote kutoka Shirikisho la Mpira wa Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kuwa ushiriki wa Ame katika mechi hiyo haukuwa halali
Hivyo, taarifa hizo za mitandaoni zisiwazuie Watanzania kuendelea kushangilia ushindi wa Taifa Stars.



