Kaka wa Pogba afungwa miaka mitatu

Joel JJ By Joel JJ β€’ 20th December 2024

Kaka wa Pogba afungwa miaka mitatu

Mathias Pogba amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya mahakama kumkuta na hatia ya kufanya njama za wizi dhidi ya nduguye, Paul Pogba

Mathias Pogba alikamatwa na kushtakiwa kwa njama ya kutaka alipwe fedha ya pauni milioni 11 ($14m) na nyota huyo wa zamani wa Juventus mwishoni mwa 2022 baada ya tukio la utekaji

Sasa, mahakama ya Paris imemkabidhi kakake Pogba kifungo cha miaka mitatu jela, huku miaka miwili ikisimamishwa

Hata hivyo, kijana huyo mwenye umri wa miaka 34 atatumikia kifungo cha mwaka mmoja kilichosalia na bangili ya kielektroniki, badala ya kufungwa jela

Pogba, 31, awali aliwaambia polisi kwamba kundi la marafiki wa utotoni, akiwemo kaka yake mkubwa Mathias, waliomba pesa kwa ajili ya "huduma za ulinzi" - kuanzia miaka 13 nyuma

Pogba mwenyewe alikiri kuwa alifikiria kustaafu mnamo 2023 wakati wa njama hii ya ulaghai lakini sasa amefarijika kufuatia uamuzi huu

Mfaransa huyo ataweza kurejea kwenye soka mwezi Machi 2025 baada ya marufuku yake ya miaka minne ya kutumia dawa za kusisimua misuli kupunguzwa hadi miezi 18 mapema mwaka huu

Kwa sasa ni mchezaji huru baada ya yeye na Juventus kukubaliana kusitisha mkataba wake

More Stories

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0
Today, READ MORE β†’
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Kane aifikia rekodi ya Lineker ya mabao 10 kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Simba yalimwa faini 10M, Mabena, Komba wakumbana na rungu la kamati ya saa 72
Today, READ MORE β†’
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Simba yamfuatilia kipa wa Zimbabwe Nelson Chadya
Today, READ MORE β†’
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Zwane kukosa mechi zilizobaki kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’
Sowah kurejea Singida BS?
Sowah kurejea Singida BS?
Today, READ MORE β†’
Mubiru atua Azam Fc
Mubiru atua Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Ligi Kuu: Yanga mikononi mwa Fountain Gate, mechi tatu kupigwa leo
Today, READ MORE β†’
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Ghana yaandikisha ushindi wa pili kwa Afrika, Uingereza yaanza kwa kishindo
Today, READ MORE β†’
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
DR Congo yapata sare ya kihistoria kombe la Dunia
Today, READ MORE β†’