Local,Normal News,Yanga

Ramovic aweka mkakati wa kuizima MC Alger kwa Mkapa

Joel JJ By Joel JJ
β€’
14 Jan 2025
Ramovic aweka mkakati wa kuizima MC Alger kwa Mkapa

Baada ya kuichapa Al Hilal bao 1-0 ugenini huko Mauritania na kurejesha matumaini ya kufuzu robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAF CL), Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesitisha sherehe na kuwataka wachezaji wasahau ushindi dhidi ya Al Hilal kwani wanakabiliwa na mechi muhimu mwishoni mwa wiki dhidi ya MC Alger

Jumamosi, Januari 18 Yanga inahitaji kushinda mchezo dhidi ya MC Alger ili kufuzu robo fainali ya CAF CL

Ramovic amesema jambo muhimu kwao ni kuelekeza nguvu katika mchezo ambao anaamini utakuwa mgumu lakini wanapaswa kutumia vyema uwanja wa nyumbani kufuzu robo fainali

"Mechi dhidi ya Al Hilal imekwisha, nimewaambia wachezaji baada ya kutoka ndani ya uwanja kila mmoja asitishe furaha yake, tunatakiwa kujiona kama hatujafanya kitu na tukitakiwa kwenda kufanya kitu kikubwa zaidi kwenye mchezo ujao wa nyumbani"

"Tunatakiwa kushinda mechi ya mwisho kwa nguvu licha ya kwamba haitakuwa rahisi, MC Alger nao wanapitia mabadiliko kwenye timu yao tofauti na walivyoanza mechi za makundi, tunachotakiwa ni kuongeza umakini kwenye mechi hii ya mwisho"

"Tutakuwa nyumbani na wao walishinda dhidi yetu wakiwa kwao, nasi tunapaswa kushinda nyumbani"

"Tumekuwa na mabadiliko mazuri ndani ya timu yetu tofauti na mechi mbili za kwanza tulizocheza na tumeanza kuimarika kwa nguvu, nawapongeza sana wachezaji wangu, lakini wanatakiwa kutambua tunakwenda kucheza mechi ngumu itakayobeba heshima yetu," alisema Ramovic

Yanga inatarajiwa kutua leo wakitokea Addis Ababa, Ethiopia ambapo timu ilitua jana kutoka Mauritania msafara ukipata muda wa kupumzika kabla ya kuunganisha ndege ya kurejea nyumbani mchana wa leo

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
47m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’