Klabu ya Yanga imetangaza msimamo wake kufuatia sintofahamu iliyojitokeza na kupelekea kuahirishwa mchezo wa ligi kuu namba 184 kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao ulipaswa kupigwa Jumamosi March 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kupitia kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika March 09, Yanga imetangaza haitashiriki mchezo namba 184 kwa tarehe yoyote ambayo itapangwa
Mabingwa hao wa Tanzania Bara wametaka kupewa haki ya USHINDI kwa mujibu wa kanuni pale timu moja inapogomea mechi
Lakini pia Yanga imetangaza kukosa imani na Mwenyekiti wa Kamati ya Uendeshaji wa Ligi Steven Mnguto na Katibu wa Kamati hiyo, Almas Kasongo wakilitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuivunja Kamati hiyo na kuteua viongozi waadilifu wenye nia njema na maslahi mapana ya mpira wa Tanzania
Katika taarifa hiyo iliyotolewa na klabu, imethibitisha Simba ilishiriki kikao cha kuelekea mchezo huo 'pre-match' kilichofanyika March 07 na katika kikao hicho haikutoa taarifa yoyote kuhusu kusudio lao la kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa usiku



