Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' iliondoka jana nchini kuelekea Morocco kwenye mchezo wa Kundi E wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya wenyeji Morocco utakaochezwa Machi 26
Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja Uwanja wa Honneur uliopo Manispaa ya d'Oujda. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma alikabidhi bendera ya Taifa kwa wachezaji wa Taifa Stars kabla ya safari hiyo kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
Morocco inaongoza kundi E ikiwa na pointi 12 baada mechi 4 ikiwa ikifuatiwa na Niger yenye pointi 6, Tanzania ikiwa ya 3 kwa kukusanya pointi 6, Zambia ikishika nafasi ya 4 kwa pointi 3 baada ya michezo 4 na Congo ipo nafasi ya 5 haina pointi
Ili kuweka hai matarajio ya kufuzu kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia, Tanzania inahitaji ushindi au hata matokeo ya sare ugenini
Fainali za Kombe la Dunia 2026 zitafanyika kati ya Juni 11 na Julai 19, 2926 zikiandaliwa kwa pamoja na Canada, Mexico na Marekani.



