Local,Normal News,Simba

Manungu afunguka baada ya kipigo cha Simba Misri

Joel JJ By Joel JJ
β€’
3 Apr 2025
Manungu afunguka baada ya kipigo cha Simba Misri

Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu amewataka mashabiki wa timu hiyo kukaa tayari kwa mchezo wa marudiano robo fainali ya kombe la Shirikisho(CAF CC) dhidi ya Al Masry ambao utapigwa Jumatano ijayo April 09 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Misri na Simba kukubali kipigo cha mabao 2-0, Mangungu alisema hayakuwa matokeo waliyotarajia lakini ari na morali iliyoonyeshwa na wachezaji katika mchezo huo, inawapa imani ya kushinda mechi ya marudiano na kufuzu nusu fainali

"Ukiangalia mchezo sisi tulitawala kwa kiasi kikubwa, ni bahati mbaya tumekosa magoli mengi ya wazi, tumetengeneza nafasi nyingi lakini hatukuwa na bahati ya kupata magoli"

"Naamini mwalimu na benchi la ufundi watakuwa na nafasi ya kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza leo"

"Hii timu tuna uwezo wa kuifunga nyumbani, hata hapa tulikuwa na uwezo wa kuifunga lakini kwa bahati mbaya tu maamuzi nayo vilvile hayakuwa sahihi upande wetu"

"Kwenye michezo hii ya kiafrika tunakubaliana na hilo lakini sasa tunawasubiri waje nyumbani tuone na sisi tutautumiaje uwanja wetu wa nyumbani"

"Jambo kubwa kwa mashabiki, wanachama na wote wanaoitakia mema Simba kuweka nguvu ya pamoja na kufanya maandalizi ya nguvu kukabiliana nao. Hii ni timu ambayo tunao uwezo wa kuitoa na kusonga mbele hatua ya nusu fainali," alisema Mangungu

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
46m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’