Kocha Simba apania ushindi Afrika Kusini

Joel JJ By Joel JJ β€’ 22nd April 2025


Kocha Simba apania ushindi Afrika Kusini

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stellenbosch katika mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali ya kombe la Shirikisho (CAF CC), Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids ameweka mkakati wa kuhakikisha kikosi chake kinashinda mchezo wa mkondo wa pili ugenini na kujihakikishia tiketi ya kucheza fainali

Jumapili, April 27 Simba itakuwa ugenini huko Durban Afrika Kusini kuwania matokeo ya kuwapeleka nusu fainali

Fadlu amesema Simba haitaenda Afrika Kusini kujilinda, bali wanakwenda kusaka ushindi na anaamini watafanikiwa

"Tumeweka msingi, lakini nyumba haijajengwa bado. Tunakwenda kwenye mchezo wa marudiano tukiwa na lengo moja tu kutafuta bao la mapema na kumaliza kazi. Hatutacheza kwa kujilinda. Hatutacheza kwa woga. Hatutaki sare. Tunataka ushindi"

Fadlu amedokeza kuwa katika maandalizi watakayofanya kabla ya safari yao kuelekea Afrika Kusini, watajikita kwenye mipango ya kushambulia kuanzia dakika ya kwanza ili kusaka bao la mapema angalau dakika kumi za kwanza litakalowapa wakati mgumu wenyeji wao.

"Tunajua Stellenbosch ni timu ya vijana wenye kasi, lakini pia wana udhaifu mkubwa wanapowekwa chini ya presha. Wanafungika. Hilo ndilo tunalotaka kulitumia. Hatutaki kuwapa nafasi ya kujipanga. Tunakwenda kuwavamia," alisema Fadlu.

Kimahesabu Simba itahitaji ushindi, sare au kama watapoteza basi sio zaidi ya tofauti ya mabao mawili na zaidi kama watafunga bao la ugenini, watawalazimu wenyeji wao kufunga kuanzia mabao matatu waweze kufuzu


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.