Ronaldinho kukiwasha New Amaan Complex

Joel JJ By Joel JJ β€’ 15th May 2025


Ronaldinho kukiwasha New Amaan Complex

Wachezaji wakongwe wa soka visiwani Zanzibar watakaovaa na mastaa wa zamani wa Brazili wamefahamika baada ya waratibu wa pambano hilo lililopewa jina la 'Match of the Legends' kuweka hadharani leo Alhamisi visiwani Zanzibar

Mechi ya kimataifa ya kirafiki baina ya wachezaji hao wa zamani wa Brazili wakiongozwa na Ronaldo de Assis Moreira 'Ronaldinho Gaucho' dhidi ya wale wa Zanzibar itafanyika Julai 27 katika Uwanja mpya wa Amaan kuanzia saa 2:00 usiku

Kwa mujibu wa Balozi wa Heshima wa Brazil wa Zanzibar, Abdulsamad Abdulrahim, mechi hiyo itawakutanisha wachezaji maarufu duniani akiwemo Ronaldinho Gaucho na wengine wa zamani kutoka Brazili, huku Zanzibar ikitarajiwa kuongozwa na Abdallah Juma Alley (Abdulwakati Juma), Murtala Ahmad Kibamba, Bakari Masoud, Nassoro Mwinyi Bwanga na wengineo

Abdulrahim amesema, nyota wote wa zamani kutoka Brazil watawasili Zanzibar Julai 26 watafanya mazoezi na vijana wenye vipaji vya soka visiwani humo.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.