Local,Normal News,Tabora

Chikola akiri mambo magumu Tabora United

Joel JJ By Joel JJ
19 May 2025
Chikola akiri mambo magumu Tabora United

February 28, 2025, ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kwa Tabora United kupata ushindi katika Ligi Kuu Bara, baada ya hapo imecheza mechi sita mfululizo sawa na dakika 540 ikiambulia vichapo huku kiungo wa kikosi hicho, Offen Chikola akitoa neno

Timu hiyo inayoshika nafasi tano kwenye msimamo wa ligi ikikusanya pointi 37, mara ya mwisho kuapata ushindi ilikuwa ni ilipoilaza Dodoma Jiji 1-0 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora, shukrani kwa bao la kujifunga la Dissan Galiwango wa Dodoma Jiji katika dakika ya 35

Baada ya hapo timu hiyo imepoteza mechi sita mfululizo ikifunga bao moja tu kupitia Offen Chikola, huku yenyewe ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara 13.

Matokeo ya mechi hizo ni; Tabora United 1-2 JKT Tanzania, Tabora United 0-3 Yanga, Pamba Jiji 1-0 Tabora United, Mashujaa 3-0 Tabora United, Singida Black Stars 3-0 Tabora United na Tabora United 0-1 KMC.

Chikola amesema matokeo wanayoyapata ni kipindi cha mpito, wao kama wachezaji wanapambana lakini ubora wa wapinzani unawaadhibu

“Hatufurahishwi na matokeo tunayoyapata, tumekuwa tukipambana kuhakikisha tunakuwa bora lakini tunazidiwa na timu pinzani, tumekaa na benchi la ufundi na kukubaliana kwa kupeana mbinu sahihi, tunaamini mechi mbili za mwisho za ligi tutarudi tukiwa imara,” alisema na kuongeza

“Tumeshindwa kufikia malengo kwa sababu ya matokeo ambayo sio rafiki kwetu, lakini hilo halituondoi kwenye kupambania timu kuwa bora, kwenye mechi mbili zilizobaki tunatarajia ugumu lakini hatutakubali kugawa pointi.”

Tabora United ipo nafasi ya tano kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 28 ikikusanya pointi 37, imebakiza mechi mbili dhidi ya Azam FC na Coastal Union ambazo zote itacheza ugenini.

Moja ya sapraizi kubwa ambazo Nyuki hao wa Tabora wamefanya msimu huu, ni kuifunga Yanga mabao 3-1, kati ya mechi 10 ambazo wameshinda hadi sasa.

Mwanaspoti

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE →
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE →
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE →
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE →
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE →
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE →
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE →
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE →
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE →
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE →