Local,Normal News,Simba, Berkane

Simba yatua Zanzibar kuikabili Berkane

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 May 2025
Simba yatua Zanzibar kuikabili Berkane

Klabu ya Simba SC imewasili salama visiwani Zanzibar ikiwa na azma ya kutwaa taji lao la kwanza la Kombe la Shirikisho barani Afrika, watakapokipiga dhidi ya RS Berkane ya Morocco katika mchezo wa mkondo wa pili wa fainali utakaofanyika Jumapili, Mei 25, kwenye dimba la New Amaan Complex.

Kikosi kizima kilichosajiliwa msimu huu kilikuwa sehemu ya msafara uliotoka Dar es Salaam mapema leo, ikiwa ni ishara ya maandalizi makini kuelekea mchezo huu wa kihistoria.

Mchezo huo wa fainali utaanza majira ya saa 10 jioni, na mara baada yake, kutafanyika hafla rasmi ya kuhitimisha msimu wa michuano ya CAF Confederation Cup (CAF CC), ikiwa ni pamoja na utoaji wa medali na zawadi kwa washindi.

Wachezaji wa Simba tayari wana uhakika wa kuondoka na medali – aidha za dhahabu endapo watashinda, au fedha iwapo matokeo yatakuwa kinyume. Hata hivyo, msimamo wa kikosi cha Wekundu wa Msimbazi uko wazi: wanataka ushindi pekee.

Ni kumbukumbu inayochoma: mwaka 1993, Simba walipoteza fainali ya Kombe la CAF kwenye Uwanja wa Uhuru, wakishuhudia wageni wakitoka na kombe mikononi mwao. Safari hii, mbele ya mashabiki wao wenyewe, Mnyama hataki kurudia makosa ya zamani.

Kwa sasa, macho yote yanaelekezwa New Amaan Complex – ambapo historia mpya inaweza kuandikwa. Simba wanapigania si tu ushindi wa mechi, bali pia heshima ya Tanzania katika anga la soka la Afrika

Wakati Simba ikiwasili Zanzibar leo, wapinzani wao RS Berkane wnatarajiwa kuwasili visiwani humo siku ya Alhamis

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
45m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’