Local,Normal News,Simba, Berkane

Rais Mwinyi kuhudhuria Simba vs Berkane, agharamia uwanja

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 May 2025
Rais Mwinyi kuhudhuria Simba vs Berkane, agharamia uwanja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi, ametoa zawadi maalum kwa timu ya Simba kwa kugharamia matumizi ya Uwanja wa New Amaan Complex uliopo Unguja utakaotumika kwa mechi ya fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho la Afrika, itakayofanyika Jumapili, Mei 25, 2025 kuanzia saa 10 jioni.

Hayo yameelezwa kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi Mawasiliano Ikulu, Zanzibar huku ikieleza uamuzi wa Rais Mwinyi unalenga kudhihirisha mapenzi yake ya dhati katika michezo pamoja na kuhamasisha ushindi kwa Simba, katika mechi hiyo ya kihistoria dhidi ya RS Berkane ya Morocco.

Imeongeza kuwa hatua hiyo pia ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar za kuunga mkono maendeleo ya michezo na kuleta hadhi ya kimataifa.

Mbali na kuruhusu matumizi ya uwanja huo bure, Rais Mwinyi amechukua dhamana ya kugharamia maandalizi yote muhimu ya uwanja kwa mechi hiyo. Aidha, fainali ya mechi hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki kutoka ndani na nje ya nchi.

Kwa kutambua uzito wa mechi hiyo kwa taifa, Rais Mwinyi ameahidi kuhudhuria fainali hiyo sambamba na Watanzania wote katika kuwaunga mkono Simba na kuhamasisha ushindi wa kihistoria.

Simba imefika fainali ya michuano hiyo ya CAF kwa kuifunga Stellenbosch kwa bao 1-0 na katika mechi ya kwanza ya fainali ilipoteza ugenini mjini Berkane, Morocco kwa mabao 2-0 na Jumapili ina kibarua cha kushinda si chini ya mabao 3-0 ili kubeba taji kwa mara ya kwanza.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
2h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
3h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
4h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
4h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
5h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
19h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
20h ago
READ MORE β†’