Local,Normal News,Yanga, Simba

Dabi ya Kariakoo: Yanga yaita mashabiki

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Jun 2025
Dabi ya Kariakoo: Yanga yaita mashabiki

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga, Ali Kamwe amewataka mashabiki na wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumatano katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya watani zao Simba

Mchezo huo wa mwisho msimu huu, utamtambulisha bingwa wa ligi kuu ya NBC ambapo atakabidhiwa kombe baada ya dakika 90 kukamilika

Kamwe amesema mpaka sasa zaidi ya tiketi 30,000 zimeuzwa akiwataka mashabiki wa Yanga kuendelea kununua tiketi takribani 25,000 zilizobaki

Kamwe amewataka mashabiki kutoingia katika mtego ww propaganda zinazofanywa na watani zao Simba ambazo amesema lengo lake ni kuinyima Yanga mapato

"Kuna propaganda za kitoto wenzetu wanafanya, siku ya jana walikuwa wakitangaza wanacheza mechi ya mwisho lakini mwishoni wanaweka nyumbani kwa maana lengo lao ni kuwafanya mashabiki wasiende uwanja wa kuamini mechi ya dabi ya Kariakoo haitakuwepo"

"Lakini niseme tu, sisi tunahitaji alama tatu zaidi kuliko mapato ya mechi hiyo. Pale uwanja hata akiingia shabiki mmoja sisi tutapambana kuhakikisha tunashinda"

"Mpaka sasa tayari tiketi 30,000 zimeuzwa hivyo niwaambie wanachama na mashabiki wetu tuchangamkie hizi tiketi 25,000 zilizobaki, hii ni mechi yetu,"alisema Kamwe

Baada ya kuhitimisha mchezo dhidi ya Dodoma Jiji visiwani Zanzibar jana, kikosi cha Yanga kimeendelea na maandalizi yake visiwani humo ambapo kitaelekea jijini Dar es salaam kesho Jumanne tayari kwa mchezo huo ambao Yanga inahitaji ushindi ili kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo

More Stories

Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
Klopp amchagua ter stegen, kipa namba moja ujerumani
5m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
34m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’