Fadlu ataka wapya sita Simba

Joel JJ By Joel JJ
•
8 Jul 2025
Fadlu ataka wapya sita Simba

Hivi karibuni, Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC ilikamilisha kikao chake jijini Dar es Salaam, ambapo mojawapo ya mambo makuu yaliyajadiliwa ni ripoti ya benchi la ufundi iliyowasilishwa na kocha mkuu Fadlu Davids.

Ripoti hiyo inalenga kutoa mwelekeo wa maboresho muhimu ya kikosi ili kuhakikisha Simba inarejea msimu ujao ikiwa na nguvu kubwa ya kuwania mataji mbalimbali.

Katika ripoti hiyo, kocha Fadlu Davids ameeleza wazi kinachohitajika kufanyika kwenye usajili ili kuondoa mapungufu yaliyoathiri utendaji wa timu msimu uliomalizika, ambapo amependekeza kuongeza wachezaji sita wa kigeni ili kuboresha nafasi muhimu ndani ya kikosi.

Miongoni mwa mapendekezo makuu yaliyotolewa na kocha ni:

  • Kuongeza nguvu katika nafasi ya Jean Charles Ahoua na kuleta mchezaji mwingine anayeweza kuhimili jukumu la namba 10, ambaye atakuwa na uwezo wa kufunga magoli na kutoa pasi za mwisho kwa wenzake.

  • Kuongeza beki wa kati mwenye uwezo mkubwa wa kukaba kwa nguvu na akili, jambo muhimu kwa kuimarisha safu ya ulinzi.

  • Kuimarisha nafasi kiungo mkabaji mwenye uwezo wa juu zaidi kuliko Yusuph Kagoma ili kuboresha udhibiti wa mchezo kati ya viungo.

  • Kuleta winga mwenye uwezo mkubwa kuliko Joshua Mutale ili kuongeza kasi na ushindani upande wa pembeni.

  • Kuongeza mashambuliaji mmoja au wawili wenye uwezo mkubwa wa kupachika mipira ndani ya wavu, wakionekana kuwa na kiwango bora zaidi kuliko Leonel Ateba na Steven Mukwala.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’, amekuwa mstari wa mbele kuanzisha bodi ya ushauri kuhusu masuala ya usajili ambayo inahusisha viongozi wa zamani wa Simba SC pamoja na wachezaji waliowahi kuitumikia klabu kwa mafanikio makubwa.

Lengo ni kuhakikisha kuna wigo mpana wa kuwafanyia tathmini wachezaji wanaopendekezwa kabla ya kusaini mikataba, na hivyo kufanya usajili wa maana na wenye manufaa kwa timu.

Viongozi wa zamani kama Geofrey Nyange ‘Kaburu’, Hassan Dalali, Ismail Aden Rage, na Evance Aveva, ambao walijulikana kwa uwezo wao wa kuleta usajili bora licha ya kukosekana kwa rasilimali nyingi, wamehusishwa tena katika mchakato huu wa usajili.

Mmoja wa wajumbe wa bodi alisema,

“Hawakushirikishwa kwenye usajili wa msimu uliopita, lakini huu unaokwenda kufanyika na wao wapo, walikuwemo kwenye kikao, wamemshauri mwenyekiti wetu nini cha kufanya ili kupata kikosi chenye ubora na tishio.”

ADVERTISE HERE

More Stories

Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
54m ago
READ MORE →
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
1h ago
READ MORE →
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
2h ago
READ MORE →
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
2h ago
READ MORE →
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
3h ago
READ MORE →
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
6h ago
READ MORE →
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
8h ago
READ MORE →
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
9h ago
READ MORE →
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
9h ago
READ MORE →
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
11h ago
READ MORE →