Hivi karibuni, Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC ilikamilisha kikao chake jijini Dar es Salaam, ambapo mojawapo ya mambo makuu yaliyajadiliwa ni ripoti ya benchi la ufundi iliyowasilishwa na kocha mkuu Fadlu Davids.
Ripoti hiyo inalenga kutoa mwelekeo wa maboresho muhimu ya kikosi ili kuhakikisha Simba inarejea msimu ujao ikiwa na nguvu kubwa ya kuwania mataji mbalimbali.





