Mabosi Simba wambakisha Camara

Joel JJ By Joel JJ β€’ 10th July 2025


Mabosi Simba wambakisha Camara

Uongozi wa Simba umepitisha mlinda lango namba moja wa timu hiyo Moussa Camara aendelee kulinda lango la wekundu hao wa Msimbazi kwa msimu mwingine, imefahamika

Camara alitua Simba msimu uliopita akitokea Horoya Ac ya Guinea, alisaini mkataba wa mwaka mmoja uliokuwa na kipengele cha kuongeza mwaka wa pili kama uongozi utaridhishwa na uwezo wake

Taarifa kutoka ndani ya uongozi imethibitisha kuwa baada ya majadiliano ya muda, mwafaka umefikiwa na golikipa bora huyo wa ligi kuu msimu uliopita, ataendelea kuitumikia Simba

Sasa Simba inapambana kukamilisha usajili wa mlinda lango mwingine Yacoub Mohammed kutoka klabu ya JKT Tanzania

Tayari Simba imeachana na magolikipa wawili Aishi Manula na Hussein Abel ambao mikataba yao imemalizika


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.