Local,Normal News,Yanga

Yanga yamthibitisha Folz

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Jul 2025
Yanga yamthibitisha Folz

Klabu ya Yanga SC imemtangaza rasmi Kocha Mkuu mpya, Romain Folz, raia wa Ufaransa, akichukua nafasi ya Miloud Hamdi ambaye aliondoka kwenda kuinoa Ismailia ya Misri.

Kocha Folz, mwenye umri wa miaka 35, ni jina linalofahamika kwenye soka la Afrika baada ya kupitia klabu na timu kadhaa, ikiwa ni pamoja na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambako aliwahi kuwa kocha msaidizi. Pia amewahi kufanya kazi kama Kocha Mkuu na Mkurugenzi wa Ufundi katika mataifa mbalimbali barani Afrika.

Kinachovutia zaidi kwenye ujio wa Folz ni ushawishi wa kocha maarufu wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger. Inadaiwa kuwa wakati wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu uliofanyika Juni 5 nchini Marekani, Wenger alimpendekeza Folz kwa Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said.

Wawili hao walikutana kwenye tukio hilo na Wenger, ambaye amewahi kufanya kazi na Folz kupitia programu maalum ya FIFA, alimshauri Hersi kuhusu uwezo wa kijana huyo.

Kwa mujibu wa taarifa, Wenger amekuwa kama mlezi kwa Folz katika nyanja ya ukocha, na kwa haiba na maono ya Rais Hersi kwa klabu ya Yanga, ushauri huo hakupuza. Mawasiliano kati ya Folz na uongozi wa Yanga yakaanza mara moja, na kwa kuwa tayari ana uzoefu barani Afrika, mchakato wa kumuajiri ulikwenda kwa urahisi.

Folz hatatua pekee, anakuja na kocha wa makipa Majdi Mnasria, raia wa Tunisia, kuimarisha benchi la ufundi la Wananchi.

Hii ni hatua nyingine kubwa kwa Yanga katika kulenga mafanikio zaidi kitaifa na kimataifa.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
1h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
2h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
2h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
3h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
5h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
18h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
19h ago
READ MORE β†’