Nyota wapya Simba waongeza mzuka Ismailia

Joel JJ By Joel JJ • 4th August 2025


Nyota wapya Simba waongeza mzuka Ismailia

Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids jana alipokea kundi la pili la wachezaji 11 wa timu hiyo waliowasili Ismailia huko Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2025/26

Wachezaji hao wameungana na kundi la kwanza lililotua Misri tangu Jumatano iliyopita leo wakiingia siku ya tano ya maandalizi

Kuongezeka kwa wachezaji hao kutaongeza mzuka katika kambi hiyo, kutokana na wachezaji watazidi kuongeza idadi kufuatia awali kuwa na wachezaji wachache.

Nyota wapya walioingia kambini jana ni pamoja na kiungo Alassane Kante, winga Mohamed Bajaber na mshambuliaji Jonathan Sowah

Wengine ni Hussein Semfuko, Morice Abraham na pia wamo Bashir Salum, Ally Mbegu na Alex Erasto kutoka timu ya vijana ya Simba (U20)

Simba itakuwa kambini kwa wiki nne kujiandaa kwa msimu mpya, ambapo inarudi Ismailia kwa mara ya pili kama ambavyo ilifanya msimu uliopita.

Wachezaji wengine ambao hawajajiunga na kambi hiyo ni pamoja na wale wanaoshiriki Fainali za Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN walioko kikosi cha Taifa Stars na kiungo  Neo Maema ambaye yuko katika kikosi cha Afrika Kusini


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.