Klabu ya Simba imefikia makubalino ya kuachana na mshambuliaji Lionel Ateba, imefahamika
Ateba aliyetua Simba msimu uliopita akitokea klabu ya USM Alger, anaondoka Msimbazi baada ya kuwatumikia Wekundu hao wa Msimbazi kwa msimu mmoja akifunga mabao 13 kwenye ligi
Baada ya kukamilisha usajili wa kiungo kiraka Naby Camara, Simba ililazimika kupunguza nyota mmoja wa kigeni
Lilikuwa ni suala la muda tu kwa maamuzi hayo kufikiwa pale Simba ilipomsajili Jonathan Sowah kutoka Singida BS na kuwa na washambuliaji watatu wa kigeni
Baada ya Ateba kuondoka, nyota wa kigeni ambao wako katika kikosi cha Simba ni Moussa Camara, Rushine De Reuck, Chamou Carabou, Alassane Kante, Mohamed Bajaber na Neo Maema
Wengine ni Joshua Mutale, Jonathan Sowah, Jean Charles Ahoua, Elie Mpanzu, Steven Mukwala na Naby Camara
Dirisha la usajili la michuano ya ligi ya mabingwa limefungwa usiku wa kuamkia leo August 16



