Local,Normal News,Simba

Mtihani wa kwanza kwa Pantev Eswatini

Joel JJ By Joel JJ
β€’
17 Oct 2025
Mtihani wa kwanza kwa Pantev Eswatini

Baada ya kutua Eswatini jana, kikosi cha Simba leo kitaanza maandalizi yake nchini humo kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) dhidi ya Nsingizini Hotspurs

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa keshokutwa Jumapili, Oktoba 19 nchini humo

Meneja Mkuu wa Dimitar Pantev atakuwa na siku mbili za kukiandaa kikosi chake kabla ya kuwavaa Nsingizini katika mchezo ambao Simba inahitaji ushindi ili kurahisisha kazi kwenye mechi ya marudiano ambayo itapigwa wiki ijayo Oktoba 26 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema wachezaji wote ambao wamesafiri na timu hiyo Eswatini wako katika hali nzuri na leo watafanya mazoezi yao ya kwanza nchini humo

Hii itakuwa mechi rasmi ya kwanza ya mashindano kwa Pantev ambaye alijiunga na Simba akitokea klabu ya Gaborone United ya Botswana aliyoiongoza hatua ya awali ya ligi ya mabingwa msiimu huu na kuondoshwa na Simba

Dakika 180 za mechi kati ya Simba dhidi ya Gaborone United, zilitosha kuwashawishi mabosi wa Simba kumuajiri kocha huyo raia wa Bulgaria ambaye aliwapa Gaborone United ubingwa wa ligi kuu msimu uliopita

Jukumu lake la kwanza sasa ni kuivusha Simba hatua ya makundi ya CAFCL msimu huu

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
48m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’