Valencia yamtaka Dieng wa Al Ahly

Joel JJ By Joel JJ β€’ 22nd January 2026


Valencia yamtaka Dieng wa Al Ahly

Klabu ya Valencia inayoshiriki ligi kuu ya Hispania 'La Liga' inatajwa kuwasilisha ofa ya €500,000 (Sh1.47 bilioni) kwa ajili ya kumsajili kiungo Aliou Dieng kutoka Al Ahly.

Hata hivyo, mabingwa hao wa Misri hawako tayari kumuachia kiungo huyo raia wa mali, wakidai bado ni sehemu muhimu ya mipango yao.

Valencia wanatarajiwa kutuma ofa nyingine nono zaidi kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo raia wa Mali.

Al Ahly watachuana na Yanga ya Tanzania siku ya kesho Ijumaa kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa (CAFCL)


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.