Aziz Ki atimkia Al Ittihad Libya

Joel JJ By Joel JJ β€’ 22nd January 2026


Aziz Ki atimkia Al Ittihad Libya

Nyota wa zamani wa Yanga Stephane Aziz Ki ameondoka Wydad AC ya Morocco na kujiunga na Al Ittihad ya Libya kwa mkataba wa miaka miwili.

Usajili wa nyota wa zamani wa Sevilla na timu ya Taifa ya Ufaransa, Wissam Ben Yedder ambao Wydad AC itaukamilisha hivi karibuni, unatajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kuishawishi klabu hiyo kumfungulia mlango wa kutokea Aziz Ki.

Al Ittihad imelipa kitita cha Dola 300,000 (Sh 825 milioni) ili kuipata saini ya kiungo huyo wa timu ya taifa ya Burkina Faso.

Klabu za Kaizer Chiefs na MC Alger nazo zilitajwa kumuwania mchezaji bora huyo wa ligi ligi kuu ya NBC 2023/24.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.