Local,Normal News,Yanga, Singida, Prisons, Azam

Yanga yaichapa Singida BS 3-0, Azam Fc yavutwa shati Mbeya

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 Mar 2026
Yanga yaichapa Singida BS 3-0, Azam Fc yavutwa shati Mbeya

Yanga imeendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Singida BS mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Airtel, Mtipa Singida.

Alikuwa ni Prince Dube aliyeibuka shujaa katika mchezo huo akifunga bao moja na kuhusika kwenye mabao mengine mawili.

Dube alifunga bao la uongozi dakika ya 41 akimalizia krosi ya Maxi Nzengeli. Dakika ya 45 Dube alifanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari na Chukwu mwamuzi akiamuru mkwaju wa penati uliowekwa kimiani na Allan Okello.

Kipindi cha pili Yanga iliendelea kutawala mchezo na kufanikiwa kuongeza bao la tatu kupitia kwa Mudathir Yahya akimalizia mpira uliotemwa na Metacha Mnata baada ya shuti la Dube.

Wananchi wamefikisha alama 32 baada ya mechi 12, wakizidi kusimika juu ya msimamo wa ligi.

Katika mchezo mwingine uliopigwa mkoani Mbeya, Azam Fc imelazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Tanzania Prisons.

Huo ulikuwa mchezo wa pili mfululizo Azam Fc wanakosa ushindi ugenini baada ya kupata sare mchezo uliopita dhidi ya Pamba Jiji.

Licha ya kuwa nyuma ya mpira kwa muda mrefu, kocha mpya wa Prisons Shadrack Nsajigwa alifanikiwa kupata alama moja muhimu nyumbani.

More Stories

APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
APR Fc yawaondosha aigles du congo kwenye caf champions league
5h ago
READ MORE β†’
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
Azam Fc yaomboleza kifo cha mlinda lango U20
9h ago
READ MORE β†’
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
Hatuna presha kuikabili Yanga - Kocha Gaborone United
11h ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
Manqoba aweka tahadhari mechi dhidi ya Gaborone United
13h ago
READ MORE β†’
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
Rasmi: JoΓ£o Pedro Atwaa Tuzo Ya Mchezaji Bora Wa Mwezi Wa Agosti
15h ago
READ MORE β†’
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
Simba inalenga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nusu fainali ni lengo kubwa
15h ago
READ MORE β†’
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
Libasse awapiga chini Max na Mwajanga, Kwenye tuzo za Mwezi.
16h ago
READ MORE β†’
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
Fei Toto azipotezea Simba, Yanga
18h ago
READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 21, Septemba 11 2026
21h ago
READ MORE β†’
UEFA champions league: matokeo ya usiku
UEFA champions league: matokeo ya usiku
1d ago
READ MORE β†’