Local,Normal News,Yanga, Prisons

Tulishakodi ndege kuelekea Tabora - Kamwe

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Mar 2026
Tulishakodi ndege kuelekea Tabora - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema klabu ilishafanya utaratibu wa kukodi ndege binafsi kuelekea mkoani Tabora kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons kabla ya mabadiliko yaliyotangazwa na Bodi ya ligi jana kuwa mchezo huo utapigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Kamwe amesema mpaka jana walikuwa wamejiandaa na safari ya kuelekea Tabora leo, lakini baada ya maelekezo ya Bodi ya ligi, safari hiyo sasa imeelekea Dodoma.

"Tumepokea barua kutoka Bodi ya ligi jana kuwa mechi itachezwa Dodoma. Kabla ya hapo tulivyoona Tanzania Prisons wanafanya maandalizi ya mechi kupigwa Tabora sisi tuliwasiliana na Shirika moja la ndege na tukaweka 'booking' ya ndege ya kutupeleka Tabora."

"Sisi kama klabu tulikuwa hatuna shida yoyote kuelekea Tabora tuliangalia ni utaratibu gani unaweza kutufikisha Tabora haraka kwani kiuhalisia isingekuwa rahisi kusafiri kwa basi na treni ilikuwa imejaa."

"Tulichokuwa tunasubiri ni taarifa kutoka Bodi ya ligi kama wangetuambia mchezo ni Tabora leo hii tungeondoka hapa kuelekea Tabora kwani taratibu zote za safari zilikuwa zimekamilika," alisema Kamwe.

Yanga imeondoka jijini Dar es salaam mapema leo wakielekea Dodoma huku wapinzani wao Tanzania Prisons ambao tayari walikuwa wamefika Tabora, wanalazimika kuelekea mkoani Dodoma

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
45m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’