Local,Normal News,Yanga, Simba, TRA, Mtibwa

Diarra afungiwa mechi tatu, mashabiki waiponza Simba

Joel JJ By Joel JJ
β€’
27 Mar 2026
Diarra afungiwa mechi tatu, mashabiki waiponza Simba

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Machi 26, 2026 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo;

Ligi Kuu ya NBC

Mechi Namba 85: Pamba Jiji FC 1-1 Simba SC

  • Klabu ya Simba imetozwa faini ya Sh. 10,000,000 (milioni kumi) kwa kosa la mashabiki wake kuwarushia chupa za maji waamuzi wa mchezo tajwa hapo juu wakati wakitoka kiwanjani baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

  • Hii ni mara ya pili ndani ya kipindi cha miezi miwili ambapo Februari 25, 2026 mashabiki wa klabu hiyo walimrushia chupa za maji mchezaji wa klabu ya Dodoma Jiji, William Edgar wakati mchezo huo ukiendelea kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

  • Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu na mazingatio ya kosa la kujirudia.

Mechi Namba 110: TRA United FC 0-0 Young Africans SC

  • Klabu ya TRA United ya mkoani Tabora imetozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la wachezaji wake kuonyeshwa kadi zaidi ya tano (5) katika mchezo mmoja, ambapo wachezaji hao walionyeshwa jumla ya kadi sita (6) kwenye mchezo tajwa hapo juu.

  • Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 47:10 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

Mechi Namba 126: Mtibwa Sugar FC 1-1 Young Africans SC

  • Mchezaji Djigui Diarra wa klabu ya Young Africans amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la kumshambulia mwamuzi wa kati wa mchezo tajwa hapo juu, mara baada ya mchezo huo kumalizika kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 41:5(5.3) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.

  • Pia, Mchezaji Djigui Diarra ametozwa faini nyingine ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la kuonesha kidole cha kati wakati akitoka uwanjani baada ya kumalizika kwa mchezo tajwa hapo juu. Diarra ametenda kosa kwa mujibu wa Kanuni ya 41:5(5.4) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji, kwa sababu kitendo hicho kinaashiria matusi na dharau.

  • Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 41:5 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.

Maamuzi kwa Waamuzi:

  • Mwamuzi wa kati, Gilbert Mrina kutoka Kilimanjaro, ameshushwa Daraja la Uamuzi kwa kosa la kushindwa kuchukua hatua stahiki kwa mchezaji Djigui Diarra kwa kitendo chake cha utovu wa nidhamu (kumshambulia mwamuzi) kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni ya 42:1(1.6) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi. Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kuwa ni kosa la kujirudia ambapo mwamuzi Gilbert Mrina alitenda kosa la aina hiyo katika mchezo namba 65 wa Ligi Kuu ya NBC (Mbeya City vs Namungo) na akaadhibiwa kwa kufungiwa mizunguko mitatu (3). Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

  • Mwamuzi msaidizi namba mbili (2), Abdulaziz Ally kutoka Arusha, amefungiwa mizunguko mitano (5) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu ambapo katika dakika ya 36 ya mchezo alinyoosha kibendera juu kuashiria kulikuwa na kosa la kuotea kabla ya mchezaji Emmanuel Mwanengo wa Young Africans kupokea pasi kutoka kwa Pacome Zouzoua. Hata hivyo, hakukuwa na kosa la kuotea kwa mujibu wa sheria za mpira wa miguu. Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42:1(1.8) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

More Stories

Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
47m ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
1h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
2h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
4h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
4h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
17h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
18h ago
READ MORE β†’