Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker amesema anatambua mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Azam Complex utakuwa mgumu lakini wamejiandaa vyema kusaka matokeo ya ushindi.
Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Barker amesema Azam Fc ni timu ngumu kufungika, takwimu zao za kutopoteza mchezo pamoja na kuruhusu mabao machache ni ishara ya uimara wao.
Barker amesema ni mchezo ambao hatarajii kuwa na nafasi nyingi lakini jambo muhimu kwa vijana wake ni kutumia vyema nafasi watakazopata.
"Nafikiri timu zote ni bora Azam Fc wameruhusu mabao machache kama ivyo kwetu hivyo itakuwa mechi ambayo itaamuliwa na mambo madogo"
"Sitarajii kuwa mchezo wenye nafasi nyingi kwa kila timu lakini jambo muhimu kwetu ni kutumia vyema kila nafasi tutakayopata"
"Natambua Azam Fc ni timu ngumu kufungika, hawajapoteza mchezo kwenye ligi hivyo lazima tuwe katika kiwango bora na ufanisi kuweza kupata ushindi"
"Tunatengeneza nafasi nyingi, naamini tutaendelea na mwendo huo, muhimu ni kuhakikisha tunazitumia nafasi hizo," alisema Barker.



