Rooney ampigia chapuo Carrick akabidhiwe mikoba Man United

Joel JJ By Joel JJ β€’ 8th May 2026


Rooney ampigia chapuo Carrick akabidhiwe mikoba Man United

Nguli wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney, ameendelea kusisitiza kuwa Michael Carrick anastahili kupewa nafasi ya kudumu ya kuinoa klabu hiyo kufuatia matokeo mazuri aliyoyapata tangu alipopewa jukumu la kuinoa timu hiyo kwa muda.

Rooney amesema Carrick ameonyesha uwezo mkubwa wa kiuongozi kwa kuirejesha Manchester United kwenye ushindani ndani ya muda mfupi, huku akieleza kuwa mafanikio yake hayapewi uzito unaostahili kwa sababu ni kocha mchanga na raia wa Uingereza.

β€œKama Manchester United wangemleta Luis Enrique au Thomas Tuchel na wakashinda michezo 10 kati ya 14 mfululizo, kila mtu angesema jambo la ajabu na kumsifia kwa kila aina ya sifa. Michael Carrick kafanya hivyo na hakuna anayemsifia kwa sababu ni kocha mchanga na ni Muingereza anapuuzwa,” alisema Rooney.

Rooney ambaye aliwahi kucheza pamoja na Carrick kwa mafanikio makubwa ndani ya Manchester United, amesema kocha huyo anaifahamu vyema DNA ya klabu hiyo na ana uwezo wa kuiongoza kwa muda mrefu.

β€œMichael Carrick ni mtu mwelevu sana, ni kocha mzuri sana na nadhani anaweza kuiongoza timu kwa muda mrefu tu. Tangu timu iwe chini yake Manchester United imepata utulivu na mashabiki sasa wanafurahia matokeo.”

Tangu apewe jukumu la kuiongoza timu hiyo mapema mwaka huu baada ya kuondoka kwa kocha wa zamani, Carrick ameiongoza United kushinda michezo 10 kati ya 14 kwenye ligi, rekodi iliyowafanya wengi kuanza kumtaja kama chaguo sahihi la kudumu Old Trafford.

Chini ya Carrick, Manchester United imefanikiwa kupata ushindi dhidi ya vigogo kama Manchester City, Liverpool FC, Chelsea FC na Arsenal FC, huku ikipewa nafasi kubwa ya kumaliza ndani ya nne bora na kurejea kwenye michuano ya UEFA Champions League msimu ujao.

Katika mahojiano tofauti, Carrick mwenyewe amesisitiza kuwa bado ameweka akili yake kwenye kuisaidia timu kumaliza msimu vizuri licha ya mjadala mkubwa unaoendelea kuhusu hatma yake ndani ya klabu hiyo.

Mashabiki wengi wa Manchester United wameonekana kumuunga mkono Carrick kutokana na mabadiliko ya haraka ya kiwango cha timu, huku baadhi wakiamini kuwa kurejesha utambulisho wa klabu hiyo kunahitaji mtu anayeifahamu vizuri historia na tamaduni za United kama Carrick.


  

More Stories

Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Azam Fc hiyooo fainali, yaichapa Yanga 3-2 nusu fainali
Today, READ MORE β†’
Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup
Azam Fc 3-2 Yanga, CRDB Cup
Today, READ MORE β†’
Ni Azam Fc vs Yanga, nani anakwenda fainali kombe la CRDB?
Ni Azam Fc vs Yanga, nani anakwenda fainali kombe la CRDB?
Today, READ MORE β†’
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande
Liverpool kuongeza dau kumnasa Diomande
Today, READ MORE β†’
Prisons wamefufua matumaini kusalia ligi kuu
Prisons wamefufua matumaini kusalia ligi kuu
Today, READ MORE β†’
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan
Tunisia yaaga kombe la Dunia kwa aibu, yapigwa 4-0 na Japan
Today, READ MORE β†’
Ivory Coast yapoteza dhidi ya Ujerumani dakika za jioni
Ivory Coast yapoteza dhidi ya Ujerumani dakika za jioni
Today, READ MORE β†’
Real Madrid yakana kuwasiliana na Olise, wakala wake
Real Madrid yakana kuwasiliana na Olise, wakala wake
Yesterday, READ MORE β†’
Simba 4-0 Coastal Union, CRDB Cup
Simba 4-0 Coastal Union, CRDB Cup
Yesterday, READ MORE β†’
Simba yaifumua Coastal Union 4-0, yatinga fainali ya CRDB Bank Cup
Simba yaifumua Coastal Union 4-0, yatinga fainali ya CRDB Bank Cup
Yesterday, READ MORE β†’