Local,Normal News,Ligi Kuu, Yanga, JKT, Fountain, Prisons, Pamba, Mtibwa

Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0

Joel JJ By Joel JJ
18 Jun 2026
Yanga yarejea kileleni Ligi Kuu ikiibamiza Fountain Gate 2-0

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Yanga SC, wamerejea kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Ushindi huo umeendelea kuonyesha ubora wa kikosi hicho katika mbio za kutetea ubingwa wao wa ligi, huku ukiwarejesha juu ya msimamo baada ya kuwa nyuma ya watani wao Simba kwa takribani saa 24 pekee.

Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare ya bila kufungana, Yanga walirejea uwanjani kwa kasi zaidi katika kipindi cha pili na kufanikiwa kupata mabao mawili yaliyowahakikishia pointi tatu muhimu.

Kiungo Pacôme Zouzoua aliifungia Yanga bao la kwanza katika dakika ya 53 kabla ya mshambuliaji Depú kuongeza la pili dakika mbili baadaye, na kuzima kabisa matumaini ya Fountain Gate kurejea mchezoni.

Katika mchezo huo, Yanga walionyesha nidhamu kubwa ya kiuchezaji pamoja na umiliki mzuri wa mpira, hali iliyowapa nafasi ya kutawala sehemu kubwa ya mchezo dhidi ya wapinzani wao waliokuwa wakicheza mbele ya mashabiki wao.

Matokeo hayo yameifanya Yanga kufikisha pointi 66 na kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC. Sasa kikosi hicho kinahitaji ushindi katika angalau mechi mbili pamoja na sare moja katika michezo iliyobaki ili kujihakikishia ubingwa wa tano mfululizo.

Pamba Jiji yashinda kwa kishindo, JKT yapigwa Isamuhyo

Katika mechi nyingine zilizochezwa leo, Pamba Jiji imeonyesha ubora wake kwa kuichapa Mtibwa Sugar mabao 4-0. Mshambuliaji Mathew Tegisi alikuwa nyota wa mchezo huo baada ya kufunga hat-trick ya pili katika Ligi Kuu msimu huu.

Hat-trick hiyo inakuja siku moja tu baada ya Mossi Ndumumwe wa Singida Black Stars kufunga hat-trick ya kwanza msimu huu.

Kwa upande mwingine, JKT Tanzania ilikumbana na matokeo yasiyotarajiwa baada ya kuchapwa bao 1-0 na Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Isamuhyo. Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na George Mpole kupitia mkwaju wa penalti katika dakika ya 45, na kuipa Tanzania Prisons ushindi muhimu katika harakati zao za ligi.

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
13h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
14h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
16h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
16h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
17h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
17h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
18h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
18h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
18h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
20h ago
READ MORE →