Matola afunguka maandalizi ya Simba kuikabili Coastal Union

Joel JJ By Joel JJ
β€’
26 Aug 2026
Matola afunguka maandalizi ya Simba kuikabili Coastal Union

Kocha Msaidizi wa Simba, Suleiman Matola, amesema kikosi hicho kimefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania dhidi ya Coastal Union utakaopigwa kesho Alhamisi katika Uwanja wa Isamuhyo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, Matola amekiri kuwa wanatarajia kukutana na upinzani mkali kutoka kwa Coastal Union, akisisitiza kuwa michezo kati ya timu hizo imekuwa na ushindani mkubwa.

Matola amesema licha ya Coastal Union kutokuwa na matokeo mazuri katika michezo yake ya hivi karibuni, kiwango cha uchezaji cha timu hiyo kinawafanya Simba kutarajia mchezo mgumu.

“Maandalizi yetu yanakwenda vizuri, nina imani haitakuwa mechi rahisi. Simba na Coastal Union ni timu zenye upinzani mkali kila zinapokutana.”

Ameongeza:

“Ukiwaangalia Coastal Union wamekuwa hawana matokeo mazuri lakini wamekuwa wakicheza vizuri na kuonyesha ushindani mkubwa. Hii inatufanya tuamini tutakuwa na mechi ngumu kesho.”

Hata hivyo, Matola amesema Simba imejipanga kuhakikisha inapata alama zote tatu katika mchezo huo.

“Lakini pamoja na ugumu wao, sisi tumejiandaa vyema kuhakikisha tunapata alama tatu katika mchezo wa kesho,” alisema Matola.

Matola azungumzia FVS na kadi nyekundu

Mbali na maandalizi ya mchezo huo, Matola pia amezungumzia matumizi ya FVS katika Ligi Kuu msimu huu, akieleza kuwa teknolojia hiyo imekuwa na umuhimu katika kuongeza usahihi wa maamuzi ya waamuzi.

Kocha huyo amesema Simba imechukua hatua mbalimbali katika mazoezi ili kuwajengea wachezaji umakini zaidi na kuepuka makosa yanayoweza kusababisha adhabu zaidi.

“Ni uamuzi muhimu kuleta FVS kwenye ligi yetu. Tumefanya kazi kubwa uwanja wa mazoezi ili kuongeza umakini kwa wachezaji na kuweza kuepuka yale ambayo yalikuwa hayaonekani na sasa yanaonekana,” alisema Matola.

ADVERTISE HERE

More Stories

Simba yamaliza uteja dhidi ya Yanga, yashinda dabi na swaga
Simba yamaliza uteja dhidi ya Yanga, yashinda dabi na swaga
32m ago
READ MORE β†’
Ronaldo asimamishwa kwa muda na shirikisho la soka Ureno
Ronaldo asimamishwa kwa muda na shirikisho la soka Ureno
5h ago
READ MORE β†’
Singida kuchunguza kadi nyekundu ya Sowah
Singida kuchunguza kadi nyekundu ya Sowah
7h ago
READ MORE β†’
Ronaldo bado mabao 20 tu afikishe 1000
Ronaldo bado mabao 20 tu afikishe 1000
10h ago
READ MORE β†’
Gas Detectors kutumika Kariakoo Derby
Gas Detectors kutumika Kariakoo Derby
14h ago
READ MORE β†’
Highlights : Coastal Union 0-2 Azam Fc
Highlights : Coastal Union 0-2 Azam Fc
22h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaizamisha Coastal Union kwa mabao 2-0
Azam FC yaizamisha Coastal Union kwa mabao 2-0
22h ago
READ MORE β†’
CFFA yairahisishia kazi Yanga Ligi ya Mabingwa
CFFA yairahisishia kazi Yanga Ligi ya Mabingwa
1d ago
READ MORE β†’
JKT Tanzania yaichapa Fountain Gate 2-1
JKT Tanzania yaichapa Fountain Gate 2-1
1d ago
READ MORE β†’
Tupo tayari kupambana na kupata matokeo dhidi ya Yanga: Neo Maema
Tupo tayari kupambana na kupata matokeo dhidi ya Yanga: Neo Maema
1d ago
READ MORE β†’