PSG wajinasua na kipigo, ikiambulia sare dhidi ya Lille

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said β€’ 29th August 2026

PSG wajinasua na kipigo, ikiambulia sare dhidi ya Lille

Paris Saint-Germain (PSG) wameepuka kipigo baada ya kufunga mabao mawili katika dakika za nyongeza na kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya Lille katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Ufaransa.

Lille walionekana kuwa kwenye nafasi nzuri ya kupata ushindi baada ya kujenga uongozi wa mabao mawili, lakini Vitinha alifunga bao la kwanza la PSG katika dakika ya kwanza ya nyongeza kabla ya nahodha Marquinhos kusawazisha kwa kichwa katika dakika za mwisho za mchezo.

Lille walifungua bao dakika ya 21 kupitia Hakon Arnar Haraldsson, huku Olivier Giroud akihusika katika maandalizi ya mabao yote mawili ya wenyeji. Lille waliongeza bao la pili dakika ya 84 kabla PSG kufanya comeback ya dakika za mwisho.

Sare hiyo imeifanya Lille kufikisha pointi nne na kukaa kileleni mwa msimamo wa awali, wakati PSG wana pointi mbili baada ya michezo miwili na bado hawajapata ushindi katika ligi msimu huu.

More Stories

Mgogoro wa Eto\'o na Waziri wa michezo Cameroon waibuka tena
Mgogoro wa Eto\'o na Waziri wa michezo Cameroon waibuka tena
Today, READ MORE β†’
Msimu mpya lakini Azam Fc ni ileile
Msimu mpya lakini Azam Fc ni ileile
Today, READ MORE β†’
PSG wajinasua na kipigo, ikiambulia sare dhidi ya Lille
PSG wajinasua na kipigo, ikiambulia sare dhidi ya Lille
Today, READ MORE β†’
Yanga yaichapa Pamba Jiji 2-0, yarudi kileleni
Yanga yaichapa Pamba Jiji 2-0, yarudi kileleni
Today, READ MORE β†’
Highlights : Yanga 2-0 Pamba Jiji
Highlights : Yanga 2-0 Pamba Jiji
Today, READ MORE β†’
Highlights : Geita Gold 2-2 Azam Fc
Highlights : Geita Gold 2-2 Azam Fc
Today, READ MORE β†’
Geita Gold na Azam FC Zagawana Pointi Bukombe.
Geita Gold na Azam FC Zagawana Pointi Bukombe.
Today, READ MORE β†’
Alvarez akosa mazoezi siku tatu katika sakata la kuhama
Alvarez akosa mazoezi siku tatu katika sakata la kuhama
Today, READ MORE β†’
Rafael LeΓ£o Ajiunga na Aston Villa kwa Mkopo.
Rafael LeΓ£o Ajiunga na Aston Villa kwa Mkopo.
Today, READ MORE β†’
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 16, August 28 2026
Xtra 90 Bets : Utabiri wa mechi 16, August 28 2026
Today, READ MORE β†’